Overview

TREATVET COMPANY LIMITED

Dealer in security services, Equipments and Training

P.O.Box 16561, Dar es Salaam Tanzania; Tel: +55789050882, +255718684992, +255716237550; Email: headoffice@ttsecurity.co.tz, Web: www.ttsecurity.co.tz

 

TANGAZO LA KAZI

Uongozi wa TT SECURITY unawatangazia wafanyakazi wote wa TT SECURITY nafasi ya kazi katika nafasi ya OPERATION MANAGER. Mfanyakazi yeyote wa TT Security na nje ya TT Security anakaribishwa kuwasilisha maombi yake kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TT Security ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili.

                                      Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo;

1.   Kwa mfanyakazi wa TT Security awe amefanyakazi kwa kipindi kisichopungua miezi 6 na kutoka nje ya TT Security awe na uzoefu usiopungua miaka 3 katika kazi ya ulinzi.

2.   Awe na elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea

3.   Awe mwenye uwezo wa kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili na kingereza kwa ufasaha.

4.   Mwaminifu na mwenye nidhamu na bidi katika kazi.

5.   Mwadilifu (asiyekuwa na kumbukumbu nyingi za makossa ya kinidhamu).

6.   Mwenye lesseni na ujuzi wa kuendesha magari na pikipiki atapewa kipaumbele zaidi.

7.   Mwombaji awe na wadhamini 3.

 

Barua za maombi ziletwe katika ofisi za TT SECURITY zilizopo masaki karibu na ofisi za umoja wa mataifa (UN).

Kituo cha daladala ni FITNESS.

Kwa anwani ifuatayo;

Meneja Mwajili,

TT Security,

s.l.p 16561,

Dar es Salaam.

 

Kwa mawasiliano:  0746 518 605.

0684 824 406.

 

         TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA UONGOZI WA TT SECURITY LEO TAREHE 15/11/2022